'Usilie kaka,'Boni Khalwale amkejeli Sossion baada ya kujiuzulu

Muhtasari
  • Wakenya wagadhabishwa na maneno yake Khalwale ya kumkejeli Sossion
  • Sossion alijiuzulu siku ya Ijumaa baada ya miaka mitatu ya mzozo wa uongozi katika muungano huo
Katibu Mkuu wa Muungano wa KNUT Wilson Sossion
Katibu Mkuu wa Muungano wa KNUT Wilson Sossion

Aliyekuwa seneta wa kaunti ya Kakamega Boni Khalwale alijipata pabaya baada ya kumkejeli Wilson Sossion baada ya kujiuzulu kwake.

Sossion alijiuzulu siku ya Ijumaa baada ya miaka mitatu ya mzozo wa uongozi katika muungano huo.

Kiongozi huyo akihutubia mkao wa wanahabari alisema siku ya Ijumaa "amezidi kiwango cha kuwasilisha matakwa ya wafanyikazi kupitia Knut," na ataangazia kutetea wafanyikazi kupitia wadhifa wake akiwa mbunge katika bunge la kitaifa.

Kupitia kwenye ukurasa wa Khalwale wa twitter alionekana kumcheka katibu huyo kwa ujumbe huu,

"Mwalimu Wilson Sosioni, usilie kaka. Mbio za sakafuni huishia ukingoni.." Aliandika Khalwale.

Hata hivyo, wananchi walionekana kuudhika na ujumbe wake kwake Sossion ambaye wengi watamkumbuka kwa kupigania haki za walimu kwa kila hali na mali.

Hizi hapa baadhi ya jumbe za wakenya;

Jsuba:Sometimes don't just comment... Teachers are the ones going to suffer... Sosion is on payroll

Felix: Daktari you will soon join him shedding tears even if they be crocodilous

oscar013: Hapo sasa ata waalimu wanalia kuliko sosion,,dynasties back to drawing board and harsh reality . Everything is vanity mwalimu

Kenn: Lakini wewe boni , hii Bangi ulianza kuvuta na guka yangu haijakutosha bado ?

Babu: Sosion was a true unionist not like the limping Khalwales , teachers those tears will haunt you