Watu 5 wakamatwa wakijaribu kuiba benki ya Prime Nairobi

Muhtasari
  • Watu 5 wakamatwa wakijaribu kuiba benki ya Prime Nairobi
  • Hata hivyo wapelelezi walifahamishwa kuhusu mpango wa wahalifu hao na kuwafumania
Pingu
Image: Radio Jambo

Watuhumiwa watano wamematwa wakati walipokuwa wakijaribu kuiba kutoka kwa  benki ya Prime katika Wilaya ya Biashara ya Kati ya Nairobi (CBD)  Ijumaa, Julai 2.

Kulingana na DCI maafisa wa polisi waliambiwa kuwa watuhumiwa walikuwa wamekomboa nyumba katika vyumba vya wageni Angle House  barabara ya Ukwala.

"kundi la wahalifu watano walioshukiwa kuwa na mpango wa kuvunja  benki ya Prime Bank OTC, walikamatwa mapema leo asubuhi. Charles Mulo, Fredrick Muuderwa, Jesse Muriuki, Gabriel Mungai na Reuben Njuka walikamatwa na timu ya polisi kutoka kituo cha polisi cha DCI na Kamukunji,"DCI Ilisema.

Hata hivyo wapelelezi walifahamishwa kuhusu mpango wa wahalifu hao na kuwafumania na kuharibu mpango wao.

Watuhumiwa hao walipelekwa katika kituo cha polisi cha Kamukunji huku waisubiri kufikishwa mahakamni.