Chagueni viongozi wenye itikadi zinazolingana na matakwa yenu-Gavana Mutua

Muhtasari
  • Gavana Mutua awashauri wakenya kuwachagua viongozi wenye itikadi
  • Katika taarifa kwenye ukurasa wake wa twitter, Mutua alisema Wakenya wanapaswa kuweka nyuma utamaduni wa kuunga vyama kwa sababu wanawakilisha makabila yao
Gavana Alfred Mutua
Image: Twitter

Gavana wakaunti ya  Machakos Alfred Mutua amewauliza Wakenya kuchagua viongozi wenye itikadi zinazolingana na matakwa yao.

Katika taarifa kwenye ukurasa wake wa twitter, Mutua alisema Wakenya wanapaswa kuweka nyuma utamaduni wa kuunga vyama kwa sababu wanawakilisha makabila yao

"Tunahitaji kujenga taasisi za kisiasa zinazotegemea itikadi na kuchagua viongozi wakizingatia kile wanachosimamia kinaambatana na hamu ya wananchi

Kenya imefikia umri kwetu kuachana na tamaa ya kuunga mkono vyama vya siasa kwa sababu zinawakilisha makabila yetu," Alisema Mutua.

Mutua alisema chama chake cha Maendeleo Chap Chap kinaamini mipango ambayo inaboresha maisha ya watu na matokeo yanayoonekana ndani ya muda mfupi.

“Nimefurahi kushiriki hayo na gavana ambaye nimemtembelea asubuhi ya leo. Gavana Kimemia ni rafiki yangu; sisi wote tulifanya kazi pamoja wakati wa Rais mstaafu Mwai Kibaki- yeye kama mkuu wa utumishi wa umma wakati mimi nilikuwa msemaji wa serikali, "Mutua alisema.

Alisema alikuwa na bahati ya kuona miradi ya kwanza ambayo Kimemia ameanzisha na kumpongeza mwenzake kwa kuweka watu mbele.