Mama wa watoto 3 apatikana ameuawa muda baada ya kumkaribisha mpenziwe kwake Naivasha

Mipira ya kondomu ambayo ilikuwa imetumika ilipatikana pale.

Muhtasari

•Mauaji ya mama huyo wa watoto watatu yalijiri baada ya kumkaribisha mpenzi wake ambaye kwa sasa hajulikani aliko.

•Jumatatu asubuhi majirani walikumbwa na tukio la kutisha ambapo mwili wa marehemu ulipatikana ndani ya nyumba yake ukiwa uchi.

crime scene 1
crime scene 1

Huzuni imetanda katika eneo la Kabati, Naivasha baada ya mwanamke mmoja wa miaka 30 kupatikana ameuwa.

Mauaji ya mama huyo wa watoto watatu yalijiri baada ya kumkaribisha mpenzi wake ambaye kwa sasa hajulikani aliko.

Polisi wanamtafuta mpenzi wa marehemu ambaye inashukiwa alienda mafichoni baada ya kutekeleza au kuhusika kwenye mauaji hayo.

Jirani mmoja wa mwanamke huyo, Jessica Njeri alisema kuwa marehemu alikuwa ameonekana katika baa moja maeneo hayo usiku wa Jumapili kabla ya kuelekea kwa nyumba yake akiandamana na mpenzi wake.

Jumatatu asubuhi majirani walikumbwa na tukio la kutisha ambapo mwili wa marehemu ulipatikana ndani ya nyumba yake ukiwa uchi.

Mipira ya kondomu ambayo ilikuwa imetumika ilipatikana pale.

Inadaiwa kuwa mlango wa nyumba ya marehemu ulikuwa umefungwa kutoka nje ndipo majirani wakaweza kufungua na kupatwa na picha ile ya kuogofya kabla ya kuita polisi wachukue mwili.

Akithibitisha tukio hilo, OCPD wa Naivasha  Samuel Waweru alisema kuwa wanamtafuta mwanaume ambaye alionekana wa mwisho kwa nyumba ya mwanamke huyo.

Waweru alisema kuwa alama za vidole zilikuwa zimechukuliwa katika eneo la tukio na mwili wa marehemu ulikuwa umepelekwa kwenye mochari huku upasuaji wa mwili ukisubiriwa ili kubaini kilichosababisha kifo hicho.