Msichana, 13, aomba binamu wake asikamatwe kwa kumpachika ujauzito, asema anampenda

Amekiri kuwa alikuwa akishiriki ngono naye kila Jumapili na hadi kulala kwake mara kwa mara.

Muhtasari

•Wahudumu wa afya katika hospitali ya Muranga General walisema kuwa viungo vyake vya uzazi havikuwa vimekomaa kwa wakati ule ikabidii ajifungue kwa njia ya upasuaji.

•Inadaiwa kuwa msichana huyo ambaye ni mwanafunzi wa darasa la sita alikuwa miongoni mwa wanafunzi bora darasani  kabla ya kudanganywa kushiriki tendo la ndoa na binamu yake.

Pregnant Student
Pregnant Student
Image: FILE

Msichana mmoja wa miaka 13  maeneo ya Murang'a amemtetea binamu yake wa miaka 24 ambaye alimpachika ujauzito.

Msichana huyo ambaye  alijifungua binti kwa njia ya upasuaji mwezi wa Mei amesema kuwa anampenda na kumjali  binamu yake ambaye ni mwendesha bodaboda na kuomba asikamatwe.

Wahudumu wa afya katika hospitali ya Muranga General walisema kuwa viungo vyake vya uzazi havikuwa vimekomaa kwa wakati ule ikabidii ajifungue kwa njia ya upasuaji.

Licha ya mashida aliyopitia, mwanadada huyo ameomba binamu yake asishtakiwe huku akisema kuwa anampenda na kumjali.

Amekiri kuwa alikuwa akishiriki ngono naye kila Jumapili na hadi kulala kwake  mara kwa mara.

Inadaiwa kuwa msichana huyo ambaye ni mwanafunzi wa darasa la sita alikuwa miongoni mwa wanafunzi bora darasani  kabla ya kudanganywa kushiriki tendo la ndoa na binamu yake.

Mapenzi kati yao yalianza kaiwa na umri wa miaka 10 huku binamu-mpenzi wake akiwa na miaka 21.

Baada ya ujauzito huo kuthibitishwa, aliarifu wazazi wake na mkutano wa familia ukapangwa.

Familia iliamua kutatua kesi hiyo nje ya mahakama huku nyanya yao akijitolea kumlea mtoto ambaye angezaliwa.Hata hivyo, binamu mwenye ujauzito alionywa kukaa mbali.

Akiwa na ujauzito wa miezi sita, familia iliamua kumhamisha mwanadada huyo kutoka Maragua mpaka Kangema ili kumuepusha na unyanyapaana kumsaidia kuendeleza masomo yake mbali na binamu yake.

Alijifungua mwezi Mei kwa njia ya upasuaji katika hospitali ya Murang'a General.

Licha ya ombi lake kuwa binamu-mpenzi wake asishtakiwe, madaktari walisisitiza kuwa mkosaji alivunja shera na anafaa kulipia matendo yake.

Mtoto aliyezaliwa alipewa jina la mamake mhasiriwa huku familia ikisema kuwa hiyo ni njia ya kuvunja uhusiano wowote na baba mtoto kuona kuwa tendo la ndoa kati ya mabinamu ni mwiko. 

Nyanya ya mwanadada huyo amependekeza adhabu kali kutekelezwa kwa mjukuu wake aliyetekeleza kitendo hicho cha aibu.

Mwanadada mhasiriwa  amesema kuwa angependa kurudi shuleni hivi karibuni ili kuendelea na masomo.