Machozi ya furaha!Mwanafunzi Bora katika mtihani wa KCSE 2020 apata msaada wa karo

Muhtasari
  • Mwanafunzi Bora katika mtihani wa KCSE 2020 apata msaada wa karo
Image: George Owiti

HABARI NA GEORGE OWITI;

Saa chache baada ya gazetti la the Star kuandika kuhusu mwanafunzi bora Faith Mumo katika mtihani wa KCPE 2020,mbunge wa Matungulu Stephen Mule alitoa msaada wa karo ya shule na matumizi anapojiunga na kidato cha kwanza.

Wanafunzi wa kidato cha kwanza wanapaswa kujiunga na kidato cha kwanza kwa muhula wao wa kwanza mnamo Agosti 2.

"Yeye ni mmoja wa wanafunzi bora katika jimbo letu, tumekubali kudhamini ada zake za shule kwa ujumla kwa mwaka mzima na miaka minne ijayo mpaka atakapomaliza

Nilizungumza na  mwalimu mkuu wa shule jioni hii na alikubali kupokea hundi na kuhakikisha Mumo anapata kila kitu anachohitaji kwa mwaka mzima

Na yote anayohitaji shuleni itachukuliwa mpaka tutakapokutana  mwaka ujao." MBunge alisema.

Machozi ya furaha yalitoka chini ya mashavu ya Mumo wakati wa sherehe. Mumo alisema alishukuru kwa msaada na kuwashukuru wote waliokuja katika maisha yake ili kuunga mkono masomo na wazazi wake.

Alikuwa na ujasiri wa kutambua ndoto yake baada ya masomo yake na aliahidi kurudi kwa jamii kwa kuunga mkono elimu ya watoto walio na nafasi.

Msaada huo ulikuja baada ya Familia ya Faith Mumo kueleza wasi wasi kwamba huenda ikashindwa kulipa karo ya shule.