'Rais analipiza kisasi kwa Naibu wake,'Kipchumba Murkomen adai baada ya DP kuzuiliwa kusafiri

Muhtasari
  • Baada ya naibu rais William Ruto kuzuiliwa kusafiri kuenda Uganda wandani wake waligadhabishwa na kitendo hicho na kuilaumu serikali kuu
  • Kulingana na mbunge Oscar Sudi alidai kwamba walizuiliwa kwa saa tano, katika uwanja wa ndege wa Wilson
Kipchumba Murkomen
Kipchumba Murkomen

Baada ya naibu rais William Ruto kuzuiliwa kusafiri kuenda Uganda wandani wake waligadhabishwa na kitendo hicho na kuilaumu serikali kuu.

Huku seneta wa Elgeyo Marakwet Kipchumba Murkomen akizungumza na kutoa hisia kwa ajili ya kitendo hicho aldai kwamba rais analipiza kisasi kwa maana alipoteza katika uchaguzi mdogo wa kiambaa mwezi uliopita.

Huu hapa ujumbe wake;

"Rais analipiza kisasi kwa Naibu wake kwa sababu ya kupoteza katika uchaguzi wa Kiambaa. Je! Ilifanyika nini kwa uchezaji mzuri?

Rais amemzuia DP kutekeleza majukumu yake rasmi na sasa anamzuia kutoka kwa shughuli zake za kibinafsi. Huu ni onyesho la ujinga la hali ya kina ya ukosefu wa usalama na ujanja," Aliandika Kipchumba.

Kulingana na mbunge Oscar Sudi alidai kwamba walizuiliwa kwa saa tano, katika uwanja wa ndege wa Wilson.

Pia alidai kwamba,ilidaiwa kwamba rais Uhuru alikataa kumpa naibu wake kibali cha kusafiri.