Mwanaume ajisalimisha kwa polisi baada ya kuua mkewe na jamaa wake wa kando alipowafumania, Nakuru

Peter Cheruiyot anaripotiwa kuchukua bodaboda hadi kituo cha polisi cha Keringet na kuripoti kuwa alikuwa ameuwa bibi yake Agnes Kirinyet (32) na Christopher Korir (40) baada ya kuwapata kitandani.

Muhtasari

•Mwanaume mmoja maeneo ya Kuresoi, Nakuru alijisalimisha kwa polisi baada ya kuua bibi yake na mwanaume aliyempata naye ndani ya chumba chao cha malazi siku ya Jumamosi.

•Kulingana na polisi, Cheruiyot alimkata Korir shingo ilhali mkewe alipatikana na vidonda vikubwa  vya kisu kichwani na kwa mkono.

Crime scene
Crime scene

Mwanaume mmoja maeneo ya Kuresoi, Nakuru alijisalimisha kwa polisi baada ya kuua bibi yake na mwanaume aliyempata naye ndani ya chumba chao cha malazi siku ya Jumamosi.

Peter Cheruiyot anaripotiwa kuchukua bodaboda hadi kituo cha polisi cha Keringet na kuripoti kuwa alikuwa ameuwa bibi yake Agnes Kirinyet (32) na Christopher Korir (40) baada ya kuwapata kitandani.

Kulingana na polisi, Cheruiyot alimkata Korir shingo ilhali mkewe alipatikana na vidonda vikubwa  vya kisu kichwani na kwa mkono.

Polisi walisema kuwa walipata mwili wa Korir ukiwa juu ya kitanda na wa Agnes ukiwa umelala sakafuni.

Eneo la tukio lilionyesha mvutano uliokuwepo.

Miili ya wawili hao ilipelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti huku upasuaji wa mwili ukisubiriwa.

Polisi walisema kuwa bado hawakuwa wamepata silaha zilizotumika kutekeleza mauaji hayo ila wanaendelea kuzitafuta.

Wanandoa wanaozozana walishauriwa kutochukua sheria mkononi ila watafute njia mbadala za kusuluhisha ugomvi.

Cheruiyot alikamatwa na alikuwa anatarajiwa kufikishwa mahakamani mnamo Jumatatu kufuatia ombi la upande wa mashtaka kutaka azuiliwe wakati uchunguzi unaendelea.

Uchunguzi kufuatia tukio hilo unaendelea.

(Utafsiri; Samuel Maina)