Mvulana wa miaka,13,ajiua baada ya kupoteza shilingi 300

Muhtasari
  • Huzuni imetanda katika kijiji cha unyula baada ta Mtoto wa miaka 13 kkujiua baada ya kupoteza shilingi 300 aliyopewa kununua vitabu
  • Kulingana na babu yake, mwanafunzi wa darasa la 5 anayeitwa Oliver aliondoka nyumbani kununua vitabu lakini hakufika dukani

Huzuni imetanda katika kijiji cha unyula baada ta Mtoto wa miaka 13 kkujiua baada ya kupoteza shilingi 300 aliyopewa kununua vitabu.

Kulingana na babu yake, mwanafunzi wa darasa la 5 anayeitwa Oliver aliondoka nyumbani kununua vitabu lakini hakufika dukani.

Oliver alikuwa ameongozana na rafiki yake kwenda dukani lakini alimdanganya kabla ya kutoweka.

"Alikuwa ameenda kwa duk na rafiki yake. Lakini alimwambia rafiki yake kuchukua baiskeli kurudi nyumbani. Aliporudi, hakumkuta Oliver. Tulifikiri alikuwa amekwenda nyumbani kwake," Daniel Wanyama alisimulia.

Baada ya siku mbili za kumtafuta mvulana huyo, alikutwa amekufa siku ya Jumatano.

Haya yanajiri wakati visa vya kujiua na mauji kuongezeka nchini bila ya kujua kwanini baadhi ya wahasiriwa hao walitenda kitendo hicho cha kusikitisha.

Kulingana na runinga ya K24, mvulana huyo alikuwa katika shule ya msingi ya Namunyweda.

Swali ambalo limesalia akilini mwa wakenya wwengi, ni kwanini watu wanajitoa uhai kama kuku au kutoa wenzao uhai?