Ndugu,2, wa Embu walifariki kutokana na majeraha ya kichwa yaliyosababishwa na kifaa butu - uchunguzi wa mwili

Muhtasari
  • Ndugu,2, wa Embu walifariki kutokana na majeraha ya kichwa yaliyosababishwa na kifaha butu
Marehemu Benson Njiru na Emmanuel Mutura
Marehemu Benson Njiru na Emmanuel Mutura
Image: HISANI

Ndugu wawili wa Embu waliokufa baada ya kukamatwa na polisi Jumapili iliyopita walifariki kutokana na kuvunjika mbavu na majeraha ya kichwa yaliyosababishwa na kifaha butu, ripoti yao ya uchunguzi wa mwili wafichua.

Upasuaji wa miili ya  marehemu ulifanyika katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Embu Level 5 Alhamisi, Agosti 5.

Miili ya Benson Njiru Ndwiga, 22, na Emmanuel Mutura Ndwiga, 19, ambao walikuwa wamepotea tangu Jumapili walipatikana Jumanne katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Embu Level 5.

Uchunguzi huo ulifanywa na Wataalamu wa magonjwa : Dk Martha Mwangi ambaye aliwakilisha familia, Dk Ndegwa aliwakilisha Kitengo cha Independent Medico-Legal (IMLU) na Dk Doris Namu ambaye aliwakilisha Hospitali ya Embu .

Wengine walikuwa Dkt Peter Muturi na Dkt Kamau Wangari.

Wakili wa familia, Muchangi Gichugu, wakati akitoa ripoti kama ilivyoamriwa na mtaalamu wa magonjwa ya familia, alisema mwili wa Benson Njiru ulikuwa na majeraha mengi kichwani na viungo vilivyovunjika.

"Benson alikuwa na majeraha mengi na hatuwezi kuelezea tu jeraha la kichwa kama sababu ya kifo," alisema.

Kwenye mwili wa Emmanuel Mutura, ripoti ilisema alikuwa na majeraha ya kichwa tu ambayo yanaonyesha angeweza kupigwa na kifaha butu.

"Familia itafuata mfumo wa haki ya jinai ili kuhakikisha tunapata haki kwa ndugu wawili Emmanuel na Benson," aliongeza.