'Niliwalea kanisani,'Lucy Wanjiru awaomboleza wanawe waliouawa Kitengela

Muhtasari
  • Lucy Wanjiru awaomboleza wanawe waliouawa Kitengela
Fredrick Muriithi, mama yake na ndugu yake mmdogo Victor Mwangi kwenye picha ya kitambo
Fredrick Muriithi, mama yake na ndugu yake mmdogo Victor Mwangi kwenye picha ya kitambo
Image: KURGAT MARINDANY

Lucy Wanjiru, mama kwa ndugu wawili Fredrick Muriithi na Victor Mwangi waliouawa huko Kitengela pamoja na binamu zao wawili amekanusha madai kwamba walikuwa majambazi.

Mama mwenye huzuni ambaye alirudi kutoka Uingereza kuwaaga wanawe kwaheri alisema walilelewa kanisani.

Akielezea nyakati zao za mwisho wakati wa mahojiano na kituo cha Runinga cha hapa nchini, Lucy alishiriki:

"Nilizungumza na kitina mimba Ijumaa tarehe 6 alipokuwa akienda kwenye sherehe ya siku ya kuzaliwa, nilimtumia pesa taslimu.

Freddie alisema hatakwenda kwenye sherehe na aliamua kubaki nyuma,"Alisema Lucy.

Siku kadhaa baadaye Lucy hakuweza kuwasiliana na wanawe kitu ambacho hakikuwa cha kawaida sana.

"Nilijaribu kuwafikia lakini sikuweza,Nilimwita mchungaji wangu nilimuomba anisaidie kuwatafuta, mchungaji aliwasubiri lakini nilipigiwa simu na kuambiwa kwamba wwameuawa,Watoto wangu sio wahalifu, niliwalea kanisani. "

Ndugu wawili na binamu zao wawili walikuwa wameenda kumtembelea jamaa huko Kitengela kwa sherehe ya nyumba na kusherehekea siku ya kuzaliwa ya mmoja wao.

Karibu saa kumi na mbili jioni, ndugu hao wawili waliondoka kutafuta mahali wangeweza kununua kuku huko Kisaju.

Wakazi ambao waliona pikipiki zikiwa zimeegeshwa kando ya ukingo wa mto walidhani wamiliki walikuwa nje kuiba ng'ombe wao.

Eneo ambalo kwa kawaida hujulikana Hifadhi ya Kitengela limekuwa na visa vya wizi wa ng'ombe.