Mtoto wa miaka 2 aaga dunia baada ya kunywa sumu,mama yuko hali mahututi

Muhtasari
  • Mtoto wa miaka 2 aaga dunia baada ya kunywa sumu,mama yuko hali mahututi
poison
poison

Mtoto wa miaka 2 aliaga dunia, mama na ndugu yake wamo hai mahututi baada ya kudaiwa  kunywa sumu, eneo la Gatina Kawangware kaunti ya Nairobi siku ya Ijumaa.

Kulingana na ripotu ambazo ziliripotiwa katika kituo cha polisi cha Muthangari, ni kuwa mama huyo alikunywa sumu na kuwapa wanawe wawili.

Mumewe aliwaambia maafisa wa polisi kwamba alipowasili nyumba saa tatu usiku aliwapata watatu hao wamekunywa sumu.

Polisi waliokimbia kwenye eneo la tukio walimpata mtoto wa mwaka mmoja miezi kumu akiwa tayari ameaga dunia.

Mama huyo wa miaka 37, na mwanawe wa miaka 12 walipelekwa katika hospitali ya Eagles Kangemi wakiwa mahututi.

Polisi walipeleka mwili wa mwendazake kwenye chumba cha kuhifadhi maiti huku wakisubiri upasuaji wa mwili.

Sababu za mama huyo kunywa pombe hazijabainika, lakini polisi walisema kwamba wamenzisha uchunguzi wa tukio hilo.

Hili ni tukio la hivi karibuni, la mauaji nchini na kuongeza idadi ya watu waliojiua.

Karibu watu 500, wameripotiwa kujiua katika miezi mitatu hadi juni, zaidi ya mwaka jana.

Mkurugenzi wa makosa ya jinai George Kinoti alisema;

"Hatujawahi rekodi idadi kubwa ya mauaji awali, na haitaji tu umakini lakini pia inahitaji hatua za kurekebisha."

Mtu mwenye umri wa chini kujiua alikuwa na miaka 9 huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 76.