Kondakta aua mwenzake kwa kisu kufuatia mzozo wa pesa jijini Nairobi

Muhtasari

•Tukio hilo lilitokea usiku wa Jumanne katika mtaa wa Ronald Ngala jijini Nairobi wakati matatu iliyokuwa ielekee upande wa Githurai 45 ilikuwa inachukua abiria.

Crime scene
Crime scene

Polisi jijini Nairobi wanawinda  kondakta mmoja aliyeua mwenzake kwa kumdunga kutumia kisu kufuatia mzozo wa pesa.

Tukio hilo lilitokea usiku wa Jumanne katika mtaa wa Ronald Ngala jijini Nairobi wakati matatu iliyokuwa ielekee upande wa Githurai 45 ilikuwa inachukua abiria.

Walioshuhudia wamesema kuwa kondakta huyo alikuwa anazozania pesa na mwezake kabla ya kuchukua kisu na kumdunga  mara kadhaa kifuani  na kumuua papo hapo.

Baada ya kutekeleza mauaji hayo kondakta yule anaripotiwa kutoweka asijulikane aliko hadi kufikia sasa.