Covid-19: Watu 970 wapatikana na corona,612 wapona, 7 waaga dunia

Muhtasari
  • Kenya imesajili visa 970 vipya vya maambukizi ya Covid-19 kutoka kwa sampuni 7,940 chini ya saa 24 zilizopita
  • Kati ya maambukizi hayo mapya wagonjwa 940 ni wakenya ilhali 30 ni raia wa kigeni,489 ni wanaume huku 481wakiwa wanawake
Image: HISANI

Kenya imesajili visa 970 vipya vya maambukizi ya Covid-19 kutoka kwa sampuni 7,940 chini ya saa 24 zilizopita.

Kati ya maambukizi hayo mapya wagonjwa 940 ni wakenya ilhali 30 ni raia wa kigeni,489 ni wanaume huku 481wakiwa wanawake.

Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 237,851 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 12.2%.

Idadi ya sampuli zilizopimwa nchini imefika 2,388,858.

Mgonjwa wa umri wa chini ana miezi 8, huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 97.

Kwa habari za kuhuzunisha watu 7 wameaga dunia kutokana na virusi vya corona, na kufikisha idadi jumla ya 4,746 ya walioaga dunia.

Vile vile watu 612 wamepona,Idadi ya waliopona sasa ni 224,882., 502 wamepona wakiwa wanapokea matibabu wakiwa nyumbani ilhali 110 wameruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hospitali tofauti.

Kuna wagonjwa 1,874 ambao wamelazwa hospitalini, 5,379 wamejitenga nyumbani.

Vile vile kuna wagonjwa 143 katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICI).

Idadi ya watu waliopokea chanjo ya corona imefika 2,807,945.