Rasmi: Rais Kenyatta ateua makamishna wapya wa IEBC waliopitishwa na bunge la kitaifa

Muhtasari

•Kenya ameteua Juliana  Whonge Cherera, Francis  Mathenge Wanderi, Irene Cherop Masit na Justus Obonyo Nyang'aya baada ya bunge la kitaifa kupitisha majina yao siku ya Jumatano.

Makamishna wapya wa IEBC walioteuliwa na rais
Makamishna wapya wa IEBC walioteuliwa na rais
Image: MAKTABA

Rais Uhuru Kenyatta ameteua rasmi makamishna wanne wapya wa tume ya mipaka na uchaguzi nchini (IEBC).

Kenya ameteua Juliana  Whonge Cherera, Francis  Mathenge Wanderi, Irene Cherop Masit na Justus Obonyo Nyang'aya baada ya bunge la kitaifa kupitisha majina yao siku ya Jumatano.

Majina ya wanne hao yamechapishwa kwenye gazeti la kitaifa na wanatarajiwa kula kiapo hivi leo (Alhamisi.

Wanne hao watahudumu kwa kipindi cha miaka sita.

Hatua hiyo inamaanisha kuwa kwa sasa IEBC imetimiza idadi ya makamishna wanaohitajika kikatiba.

Kwingineko rais pia ameteua makamishna watano wa tume ya kuajiri waalimu nchini (TSC)  na kumaliza shida iliyokuwepo.

Rais ameteua Nicodemus Ojuma Anyang, Christine Kahindi, Anneta Wafukho na Salesa Adano, na Sharon Chelagat kujiunga na TSC kwa kipindi cha miaka sita.