Matiang'i azindua kaunti ndogo mpya Laikipia katika juhudi za kukabiliana na ukosefu wa usalama

Tangazo lilichapishwa kwenye gazeti la kitaifa

Muhtasari

•Hatua hiii itawezesha huduma za serikali na mashirika ya usalama kufikia wakazi wa maeneo ya Sipili na Ng'arua ambayo yameonekana kutengwa kwa muda.

Image: HISANI

Waziri wa masuala ya ndani Fred Matiang'i amezindua kaunti ndogo mpya maeneo ya Laikipia katika juhudi za kujaribu kukabiliana na ukosefu wa usalama pande hizo.

Matiang'i alitangaza kuzinduliwa kwa kaunti ndogo ya Kirima siku ya Alhamisi kupitia gazeti la kitaifa.

"Katika jaribio la kuboresha utekelezaji wa kazi za serikali, waziri wa masuala ya ndani na uratibu wa kazi za serikali amezindua kaunti ndogo ya Kirima  mnamo Septemba 9, 2021" Tangazo hilo lilisoma. 

Hatua hiii itawezesha huduma za serikali na mashirika ya usalama kufikia wakazi wa maeneo ya Sipili na Ng'arua ambayo yameonekana kutengwa kwa muda.

Kaunti ndogo ya Kirima inatarajiwa kupata kamanda wa polisi , hatua ambayo itasaidia kutatua masuala ya usalama.

Siku za hivi karibua ghasia kubwa zimekuwa zikishuhudiwa katika kaunti ya Laikipia ambapo waliojihami kwa bunduki wamekuwa wakivamia wakazi pamoja na maafisa wa polisi.