Hofu Dagoretti baada ya mwanamke kuua mumewe kwa kumdunga kisu kufuatia mzozo wa kinyumbani

Muhtasari

•Polisi waliweza kumkamata mshukiwa kutoka mafichoni yake maeneo hayo ya Dagoretti na kumzuilia

Crime scene
Crime scene

Polisi jijini Nairobi wanazuilia mwanamke mmoja anayedaiwa kuua mumewe kwa kumdunga na kisu kufuatia mzozo wa kinyumbani .

Peninah Wanjiru 33, anadaiwa kutoa kisu na kumdunga mumewe George Ogamo 27, kisha kujaribu kutoroka walipokuwa wanazozona  nyumbani kwao katika kijiji cha Mukarara eneo la Dagoretti, Nairobi. 

Polisi waliweza kumkamata mshukiwa kutoka mafichoni yake maeneo hayo ya Dagoretti na kumzuilia

Bado haijabainika wazi kiini cha mzozo uliosababisha maafa hayo huku uchunguzi zaidi ukiendelea kufanyika ili kupata majibu.