Bei ya mafuta inapaswa kupunguzwa mara moja- Raila asema

Muhtasari
  • HUku wakenya na baadhi ya viongozi wakilalamika kwa ajili ya ongezo ya baei ya mafuta kinara wa ODM Raila Odinga amevunja kimya chake kuhusiana na swala lilo hilo
Kinara wa ODM Raila Odinga
Image: Maktaba

HUku wakenya na baadhi ya viongozi wakilalamika kwa ajili ya ongezo ya baei ya mafuta kinara wa ODM Raila Odinga amevunja kimya chake kuhusiana na swala lilo hilo.

Raila alisema siku ya Alhamisi kwamba Wakenya wamekuwa wakipambana kuweka chakula mezani tangu mwanzo wa janga la cprona  na sasa maisha ya wananchi yameendelea kuwa magumu zaidi baada ya ongezeko la bei ya mafuta.

"Wakenya ambao wamekuwa wakihangaika kuweka chakula mezani tangu mwanzo wa janga la corona sasa wanasimama kuwa na shida yao ya pamoja kuzidishwa na kuongezeka kwa bei ya mafuta.

Bei inapaswa kushushwa mara moja ili kuwavutia Wanainchi wa kawaida."

Hisia zake zinakuja wakati Wakenya wanaendelea kuelezea kutoridhika kwao juu ya bei kubwa ya mafuta, ambayo kwa hakika itasababisha gharama kubwa ya maisha.

Mapema Alhamisi, DP William Ruto alisuta serikali juu ya ongezeko la mafuta, akitaka Wizara ya Nishati kushirikiana na wakala husika na Kamati za Bunge kushughulikia kupanda kwa bei ya mafuta.

DP alisema haya Alhamisi alipokutana na viongozi  kutoka Jimbo la Kandara katika makazi yake ya Karen.

Ruto alisikitika kwamba viongozi walikuwa wakikimbia majukumu yao kwa kujihusisha na siasa ambazo hazikuwaongeza thamani yoyote kwa watu.