Covid-19:Watu 511 wapatikana na corona,273 wapona,12 waaga dunia

Muhtasari
  • Watu 511 wamepatikana na maambukizi ya Covid-19 kutoka kwa sampuni 7,955 chini ya saa 24 zilizopita
  • Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 245,337 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 6.4%
Waziri Mutahi Kagwe
Waziri Mutahi Kagwe
Image: MOH

Watu 511 wamepatikana na maambukizi ya Covid-19 kutoka kwa sampuni 7,955 chini ya saa 24 zilizopita.

Kati ya maambukizi hayo mapya wagonjwa 488 ni wakenya ilhali 23 ni raia wa kigeni,263 ni wanaume huku 248 wakiwa wanawake.

Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 245,337 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 6.4%.

 

Idadi ya sampuli zilizopimwa nchini imefika 2,478,820.

Hata hivyo watu 12 wameaga dunia kutokana na virusi vya corona, na kufikisha idadi jumla ya 4,961 ya walioaga dunia.

Aidha watu 273 wamepona,Idadi ya waliopona sasa ni 235,469, 168 wamepona wakiwa wanapokea matibabu wakiwa nyumbani ilhali 105 wameruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hospitali tofauti.

Kuna wagonjwa 1,483 ambao wamelazwa hospitalini, 3,323 wamejitenga nyumbani.

Vile vile kuna wagonjwa 121 katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICI).