Mzee aenda mafichoni Kitui baada ya kuua mwajiri wake kwa kumdunga kisu kifuani

Muhtasari

•Mshukiwa anadaiwa kuchukua kisu katika duka la nyama alikokuwa anafanya kazi na kumdunga mwajiri wake kifuani kabla ya kukimbia eneo la tukio.

Crime scene
Crime scene

Polisi katika kaunti ya Kitui wanawinda mwanaume wa miaka 61 ambaye aliua mwajiri wake kwa kumdunga kisu kufuatia mzozo usiojulikana.

Inaripotiwa kwamba Maanzi Kitemi alitoweka punde  baada ya kuua John Muneni Kiteme ambaye alikuwa anamiliki duka la nyama maeneo hayo.

Wawili hao  walikuwa wanapiga maji katika baa moja mjini Kamuwongo wakati mzozo uliopelekea maafa yale ulitokea.

Mshukiwa anadaiwa kuchukua kisu katika duka la nyama alikokuwa anafanya kazi na kumdunga mwajiri wake kifuani kabla ya kukimbia eneo la tukio.

Mwili wa marehemu ulipelekwa mochari huku harakati za kusaka mshukiwa ziking'oa nanga.