Butwaa baada ya vifaa vya uchawi vikiwemo nyoka, chupi na pembe ya nyati kupatikana Busia

Muhtasari

•Mhubiri aliyetambulishwa kama Steven Wanyonyi kutoka kanisa ya Pentecost alikuwa amealikwa na familia moja ambayo ilikuwa imekabiliwa misiba mbalimbali ikiwemo magonjwa na vifo.

Image: KNA

Habari na KNA Milton Ajiambo/Absalom Namwalo

Butwaa kubwa iliwapiga wakazi wa kijiji cha Emuramia, kaunti ya Busia baada ya  vifaa vya kutisha vinavyoaminika kutumika kuendeleza uchawi kufukuliwa na mhubiri mmoja.

Inaripotiwa kuwa vifaa hivyo ikiwemo pembe ya nyati, chupi na nyoka iliyokuwa imewekwa ndani ya chungu chenye mashimo matatu zilitolewa ndani ya mto.

Mhubiri aliyetambulishwa kama Steven Wanyonyi kutoka kanisa ya Pentecost alikuwa amealikwa na familia moja ambayo ilikuwa imekabiliwa misiba mbalimbali ikiwemo magonjwa na vifo.

Wanakijiji waliridhishwa na operesheni hiyo wengine wakieleza jinsi wamekuwa wakiumia kwa muda kutokana na uchawi ambao umeshamiri katika kijiji hicho.

Mzee mmoja wa kijiji aliyetambulishwa kama Albert Butoro alilaani wale ambao wanaendeleza uchawi na kudai kwamba wanazorotesha maendeleo.

Aliwaomba watubu dhambi zao na wakubali kuokoka.