MoH imepokea kundi la mwisho la sindano maalum za chanjo ya Pfizer

Muhtasari
  • Moh imepokea kundi la mwisho la sindano maalum za chanjo ya Pfizer
  • Wizara ya Afya inasema sasa itaanza kupeana chanjo ya Pfizer kuanzia Jumatatu
Image: MoH

Kundi la mwisho la sindano maalum kutumiwa kwa chanjo za Pfizer liliwasili nchini siku ya JUmapili asubuhi.

Hii sasa inakamilisha kundi la sindano maalum milioni 2.2 kutoka kwa serikali ya Marekani ambayo itatumika katika kusimamia chanjo.

Wizara ya Afya inasema sasa itaanza kupeana chanjo ya Pfizer kuanzia Jumatatu.

Hii inatarajiwa kuongeza mpango wa chanjo ambayo inalenga kuwa Wakenya milioni 10 ifikiapo mwezi wa Desemba mwaka huu.

Kenya ilipata kundi la kwanza la sindano maalum siku ya Jumamosi.

Image: MoH

Sindani hio zilipokewa na maafisa wa  Wizara ya Afya baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) saa saba unusu mchana.

 Jumla ya sindano maalum ambazo zilitarajiwa na serikali zilikuwa milioni 2.2.