Jambazi mmoja auawa, wawili watoroka na majeraha ya risasi baada ya kupatikana wakivamia mwanamke Nairobi

Muhtasari

•Majambazi wale walipopatikana wakitekeleza wizi walianza kutoroka huku wakifyatua risasi kuelekezaa kwa maafisa  wale.

•Mmoja wa majambazi wale alipata majeraha mabaya na kufariki kwenye makabilianoa yale huku wenzake wawili ambao pia walipatwa na risasi kadhaa wakijitupa kwenye maji taka na kuogelea kuelekea eneo la Njiru.

crime scene 1
crime scene 1

Maafisa wa DCI jijini Nairobi waliwapiga risasi washukiwa watatu wa wizi wa mabavu  na kuua mmoja wao papo hapo huku wawili wengine wakiweza kutoroka na majeraha ya risasi mwilini.

Kulingana na DCI, watatu hao walikuwa wanashambulia mwanamke aliyekuwa anaelekea nyumbani kwake asubuhi ya Jumapili wakati maafisa walitua katika eneo la tukio.

Maafisa kutoka kituo cha Dandora ambao walinusuru mwanamke huyo kutoka mikononi mwa majambazi hao walikuwa wamepokea ripoti kuhusu genge ambalo lilikuwa linawahangaisha wakazi na kuwaibia vitu vya thamani.

Majambazi wale walipopatikana wakitekeleza wizi walianza kutoroka huku wakifyatua risasi kuelekezaa kwa maafisa  wale.

Mmoja wa majambazi wale alipata majeraha mabaya na kufariki kwenye makabilianoa yale huku wenzake wawili ambao pia walipatwa na risasi kadhaa wakijitupa kwenye maji taka na kuogelea kuelekea eneo la Njiru.

Juhudi za kuwasaka wawili hao zinaendelezwa na wapelelezi wa DCI kwa ushirikiano na polisi kutoka kituo cha Buruburu.

Mwanamke ambaye alikuwa anashambuliwa na majambazi wale wakati maafisa waliwasili alizindikishwa na kupelekwa nyumbani. Hakuwa ameumia kwa namna yoyote.