Raila akanusha madai kwamba huwa anazuru eneo la Magharibi ili kutafuta kura tu

Alisema kuwa madai hayo kutoka kwa baadhi ya wanasiasa ni mabaya na ya uongo.

Muhtasari

•Waziri mkuu wa zamani huyo alikumbusha wafuasi wake kwamba ingawa ako na uhusiano mzuri wa kazi na rais Uhuru, haimaanishi kwamba serikali ni yake.

•Aliahidi kwamba iwapo atachaguliwa atahakikisha kuwa eneo hilo limestawi kiuchumi kwa kuhakikisha kuwa masuala ya kiwanda cha sukari na  la mkasa wa mafuriko katika maeneo mbalimbali kama Budalang'i yameangaziwa

Raila Odinga pamoja na viongozi wengine katika mazishi ya Margret Nandalwe
Raila Odinga pamoja na viongozi wengine katika mazishi ya Margret Nandalwe
Image: JOHN NALIANYA

Kinara wa ODM Raila Odinga amekanusha madai kwamba huwa anatembelea eneo la Magharibi kwa minajili ya kutafuta kura tu  alafu anapeleka miradi yote ya maendeleao Nyanza. 

Raila alisema kuwa madai hayo kutoka kwa baadhi ya wanasiasa ni mabaya na ya uongo.

"Siwezi kutenga eneo la Magharibi ama eneo lolote nchini. Miradi ya hivi karibuni ambayo imezinduliwa Nyanza kama bandari haingeweza kuletwa katika eneo la Magharibi kwa sababu eneo hili kwa sababu hakuna ziwa kama Kisumu" Raila alisema.

Alisema kwamba mpango wa mradi huo wa bandari ulifanywa miaka kadhaa iliyopita.

Odinga alikuwa akizungumza katika hafla ya mazishi ya Margret Nandalwe, mama ya mwanasiasa Moses Nandalwe.

Alisema kuwa mradi wa reli ambao ulizinduliwa Kisumu unaenda hado Butere na ingine kutoka Nakuru kuenda hadi mpaka wa Malaba.

Odinga alisema kwamba alikuwa waziri wa barabara wakati wa utawala wa Mwai Kibaki na akaanzisha ujenzi wa barabara kadhaa muhimu katika eneo la Magharibi. Miongoni mwa barabara hizo ni pamoja na ile ya kutoka Kisumu-Kakamega na kutoka Kakamega-Kitale.

Waziri mkuu wa zamani huyo alikumbusha wafuasi wake kwamba ingawa ako na uhusiano mzuri wa kazi na rais Uhuru, haimaanishi kwamba serikali ni yake.

"Bado tuko katika upinzani na safari yetu ya kuchukua usukani wa taifa hili bado haijatimia" Raila alisema.

Aliahidi kwamba iwapo atachaguliwa atahakikisha kuwa eneo hilo limestawi kiuchumi kwa kuhakikisha kuwa masuala ya kiwanda cha sukari na  la mkasa wa mafuriko katika maeneo mbalimbali kama Budalang'i yameangaziwa.

Bosi wa COTU Francis Atwoli alitahadharisha viongozi ambao wanaunga naibu rais William Ruto mkono watapoteza viti vyao.

(Utafsiri: Samuel Maina)