Mwalimu wa sekondari ashtakiwa kwa kutongoza, kubusu na kugusa mwanafunzi vibaya Nairobi

Muhtasari

•Kulingana na karatasi za mahakama, Otieno anadaiwa kutumia wadhifa wake kama mwalimu kutongoza mwanafunzi wake kwa kumguza matiti na kumbusu.

•Otieno alisimamishwa kazi na kisha kukamatwa na kufikishwa mahakamani ambapo alikanusha mashtaka dhidi yake na kuachiliwa kwa dhamana ya shilingi 100,000. 

court
court

Habari na Clause Masika

Mwalimu wa shule moja ya upili jijini Nairobi alifikishwa katika mahakama ya Kibera siku ya Jumanne na kushtakiwa kwa kosa la kutumia wadhifa wake vibaya.

Dennis Otieno anatuhumiwa kujaribu kutongoza msichana wa miaka 15, kumguza vibaya na kumbusu kwa nguvu. Anadaiwa kutekeleza makosa hayo kati ya mwezi Julai mwaka jana na mwezi Septemba mwakani katika mtaa wa Dagoretti, Nairobi.

Kulingana na karatasi za mahakama, Otieno anadaiwa kutumia wadhifa wake kama mwalimu kutongoza mwanafunzi wake kwa kumguza matiti na kumbusu.

Inaripotiwa kwamba Otieno alihudhuria darasa lake la Kiswahili akiwa amefadhaika na kukasirika, jambo ambalo lilimtia wasiwasi mwanafunzi yule na baadae ktpitia mtandao wa WhatsApp akamuuliza kuhusu kilichokuwa kinamsumbua.

Mshukiwa  kwanza alimpongeza mwanadada huyo kwa namna alivyokuwa amevaa sare yake ya shule kisha akamueleza alivyokuwa amesikitishwa na jinsi wanafunzi walikuwa wanahusiana na walimu haswa wa kiume.

Isitoshe, Otieno anadaiwa kumtumia mwanafunzi huyo ujumbe akimhakikishia kuwa alimpenda sana. Hata hivyo, jumbe ambazo mwanafunzi yule alipokea kutoka kwa Otieno hazikupatikana kwa simu yake kwani alikuwa amefuta ila zilipatikana kwa simu ya mshukiwa.

Inasemekana kwamba Otieno aliendelea kumtongoza mwanafunzi huyo hadi tarehe 6 Septemba ambamo alimshawishi aandamane naye hadi ofisini ambapo anaripotiwa kufunga mlango, kumlaza kwenye ukuta, kumbusu na kuanza kumgusa vibaya.

Muda mfupi baadae mwanafunzi mwingine anadaiwa kubisha mlango na hapo ndipo Otieno alikimbia kwa dawati iliyokuwa karibu na mlango na kujifanya kama kwamba alikuwa anasoma kitabu. Mhasiriwa naye akajificha nyuma ya mlango.

Mhasiriwa ambaye alikuwa amejawa na hofu alimsihi mwanafuzi mwenzke kumpeleka darasani ambako alimueleza yaliyokuwa yametendeka. Baadae wakaripoti kwa mwalimu mwingine ambaye alifahamisha mama ya mhasiriwa na kesi hiyo ikaripotiwa kwa polisi.

Otieno alisimamishwa kazi na kisha kukamatwa na kufikishwa mahakamani ambapo alikanusha mashtaka dhidi yake na kuachiliwa kwa dhamana ya shilingi 100,000. Kesi hiyo itatajwa tena baadae mwezi huu.