Wawili wapoteza maisha kwenye mkasa wa moto Mlango Kubwa

Muhtasari

•Moto huo ulianza kwa chumba kimoja kisha kuenea kwa takriban vyumba vingine hamsini mida ya saa nane usiku wa kuamkia Ijumaa.

Moto mkubwa
Moto mkubwa
Image: WIKIPEDIA

Habari na Cyrus Ombati

Watu wawili walipoteza maisha yao na mwingine mmoja hajulikani alipo wakati moto mkubwa uliteketeza nyumba kadhaa katika mtaa wa Mlango Kubwa jijini Nairobi.

Moto huo ulianza kwa nyumba moja na kuenea kwa takriban nyumba zingine za mabati hamsini mida ya saa nane usiku wa kuamkia Ijumaa.

Polisi walisema kuwa waliweza kuuthibiti moto huo na kupata mwili wa mwanaume mmoja na mtoto. Hata hivyo, mwanamke mmoja mkazi wa eneo hilo hakuonekana.

Naibu bosi wa polisi jijini Nairobi James Mugera alisema kuwa bado hawajaweza kuthibitisha chanzo cha moto huo.

Mugera alisema kuwa kuna hofu huenda idadi ya waliofariki ikaongezeka wanapoendelea na juhudi za kuokoa maisha.

Miili ya wawili ambao walipoteza maisha ilipelekwa katika mochari ya City.