Uingereza yaonya raia dhidi ya kusafiri kwenda Mandera, Lamu na Garissa

Muhtasari
  • Uingereza yaonya raia dhidi ya kusafiri kwenda Mandera, Lamu na Garissa
Image: Laban Waloga

Uingereza imetoa ushauri wa usafiri dhidi ya safari zote isipokuwa muhimu kwa kaunti za Mandera, Garissa na Lamu nchini Kenya.

Katika ushauri huo uliotolewa siku ya Ijumaa, Uingereza ilisema uamuzi huo ulifanywa kwa kuzingatia hali ya usalama katika eneo hilo.

Hapo awali Uingereza ilikuwa imeshauri dhidi ya safari zote isipokuwa muhimu kwa maeneo yaliyo ndani ya kilomita 60 kutoka mpaka wa Kenya na Somalia.

Lakini sasa pia wanashauri dhidi ya safari zote isipokuwa muhimu kwenda Kaunti ya Mandera ukiondoa kaunti ndogo ya Mandera Magharibi.

Pia wametoa ushauri dhidi ya safari zote isipokuwa muhimu kwenda Kaunti ya Garissa Mashariki (hadi kilomita 20 kaskazini-magharibi), Kaunti ya Lamu (bila kujumuisha Kisiwa cha Lamu na Kisiwa cha Manda) na maeneo ya Kaunti ya Tana River kaskazini.

Haya yanajiri saa chache baada ya rais Uhuru Kenyatta kuagiza taasisi za usalama wa ndani kuongeza umakini na ufuatiliaji kote nchini kufuatia hali ya usalama inayoendelea katika eneo hilo.

Mkuu wa Nchi alitoa maagizo hayo wakati wa kikao cha Ijumaa cha Baraza la Usalama la Kitaifa.

Uhuru alitoa agizo hilo huku maafisa wa polisi wakitoa fadhila ya Sh50m kwa washukiwa watano wa ugaidi.

Polisi walitoa fadhila kwa mfungwa wa ugaidi Elgiva Bwire, Salim Rashid Mohammed, Mohammad Abubakar, Barigi Abdikadir Haila na Trevor Ndwiga.