Msichana wa miaka 14 akimbia nyumbani kuepuka ndoa ya mapema

Muhtasari

•Mtoto huyo alisema babake alikuwa na mipango ya kumuoza kwa mwanamume mwenye umri wa miaka hamsini ambaye amekuwa mgonjwa tangu arejee kijijini kutoka Nairobi.

Msichana wa miaka 14 akimbia nyumbani kuepuka ndoa ya mapema
Msichana wa miaka 14 akimbia nyumbani kuepuka ndoa ya mapema
Image: ROBERT GITHU

Msichana wa miaka 14 ambaye alitoroka nyumbani siku mbili zilizopita baada ya kujua mipango ya babake ya kumuoza amepelekwa katika kituo cha uokoaji wa Watoto cha Suguta-marmar na mamake kufikishwa mahakamani.

Mtoto huyo alisema babake alikuwa na mipango ya kumuoza kwa mwanamume mwenye umri wa miaka hamsini ambaye amekuwa mgonjwa tangu arejee kijijini kutoka Nairobi.

Aliongeza kuwa babake alimtoa shuleni alipokuwa darasa la tatu kuchunga mbuzi.

Afisa Mkuu katika kituo cha Polisi cha Maralal (OCS), Johnstone Musyoki, alisema kuwa msichana huyo alitembea kilomita 40 kutoka nyumbani kwao Suguta marmar hadi Maralal ambako aliripoti kisa hicho.

“Baada ya kutoa taarifa maafisa wa polisi walielekea nyumbani kwake kumsaka baba lakini hakuwapo ndipo tukamkamata mama huyo ambaye alifikishwa mahakamani leo,” alisema.

Baada ya kusikiliza kesi yake, Hakimu Mkuu Mwandamizi wa Maralal, James Wanyanga, aliiagiza Ofisi ya Watoto kufanya hivyo.

(Utafsiri: Samuel Maina)