Mshukiwa aliyempiga askari risasi katika klabu kujibu mashtaka ya mauaji

Muhtasari
  • Upande wa mashtaka sasa unapanga kuboresha mashtaka kuwa mauaji
  • Amekanusha mashtaka matatu ya kujaribu kuua katika klabu hiyo kando ya barabara ya Thika
Dickson Mararo
Image: Maktaba

Mmiliki wa bunduki  anatazamiwa kukabiliwa na shtaka la mauaji baada ya mmoja wa waathiriwa aliowafyatulia risasi katika klabu moja kando ya barabara ya Thika, Nairobi kufariki hospitalini miezi minne baadaye.

Mwathiriwa ambaye ni afisa wa polisi aliyetambuliwa kama Festus Musyoka alifariki hospitalini Jumanne ambako amekuwa tangu Julai 2 alipopigwa risasi shingoni na mshika bunduki Dickson Mararo.

Tukio hilo lilitokea katika klabu hiyo baada ya mtu anayedaiwa kuwa ni mpenzi wa mwanamke kijana kugeuka na kuwa majibizano ya risasi na kuwajeruhi watu watatu wakiwemo polisi wawili.

Mkuu wa polisi wa Starehe Julius Kiragu alisema maafisa wanaoshughulikia kesi hiyo watatoa taarifa kwa upande wa mashtaka ipasavyo ili kubadilisha mashtaka.

Majibizano hayo ya risasi yalihusisha Mararo, ambaye alikuwa raia aliyepewa leseni ya kubeba silaha na ambaye anadaiwa kuwapiga risasi watatu hao ambao baadaye walijisalimisha kwa polisi.

Bunduki ya Mararo, bastola ya Glock iliyokuwa na risasi 38, ilitwaliwa hadi kesi iamuliwe.

Aliachiliwa kwa dhamana ya Sh5 milioni pesa taslimu au bondi ya Sh10 milioni. Hajamudu kuondoka gerezani kwa sababu dhamana ya pesa taslimu ilikuwa kubwa mno.

Alihamia kortini kutaka masharti ya dhamana yapunguzwe.

Mnamo Oktoba, alituma maombi kwa hakimu Esther Kimilu kukagua tena masharti ya dhamana ili aweze kutoka gerezani na kuhudhuria kesi yake akiwa nje.

Mnamo Agosti 6, mahakama ilisikia kwamba Mararo, ambaye anakabiliwa na mashtaka ya kujaribu kuua, aliwapiga risasi na kuwajeruhi wahasiriwa wake watatu katika Quiver Lounge usiku wa Julai 2.

Upande wa mashtaka sasa unapanga kuboresha mashtaka kuwa mauaji.

Amekanusha mashtaka matatu ya kujaribu kuua katika klabu hiyo kando ya barabara ya Thika.

Hati ya mashtaka inasema Mararo alijaribu kusababisha vifo vya askari polisi Fetus Musyoka wa kitengo cha Starehe na Lawrence Muturi wa Kasarani na mhudumu Felistas Nzisa.

Musyoka alipata majeraha ya risasi shingoni pamoja na mwenzake kutoka kitengo cha uhalifu mdogo wa Kasarani, Muturi ambaye alipigwa risasi mkononi.