Sipangwingwi!DP Ruto asema huku akilaani vyama vya kisiasa vya kikabila

Muhtasari
  • Naibu Rais William Ruto amesema vyama vya kikabila havifai kupewa nafasi katika nafasi ya kisiasa ya Kenya
DP Ruto alaani vikali vyama vya kisaisa vya kikabila
Image: DP Ruto,TWITTER

Naibu Rais William Ruto amesema vyama vya kikabila havifai kupewa nafasi katika nafasi ya kisiasa ya Kenya.

Alivitaja kuwa vikwazo vikubwa zaidi vya maendeleo ya Kenya kwani wanazidisha chuki, migawanyiko na ukabila.

Ruto alisema haiwezekani kuunganisha nchi ikiwa "kila mtu ana chama chake cha kisiasa kutoka kona yake, kutoka kwa jamii yake, kutoka eneo."

"Siasa ya ukabila ndio imerudisha Kenya nyuma na nafasi yetu safari hii tuondoe, tumalize na tuzike siasa ya ukabila katika taifa letu la Kenya

Njia ya kuondoa siasa ya ukabila katika taifa letu la Kenyanni kuhakikisha sote tumeungana kwa chama ambayo inaunganisha wakenya wote. Chama ya kazi ni kazi. Chama ya UDA.

Nataka wajue vile wakenya wamesema hawapangwingwi. Mimi pia kama hustler nataka niwaambie sipangwingwi. Wao wanaweza kupangwa na deep state ama na system lakini sisi hatupangwingwi," Ruto alisema.

Alizungumza Jumatatu katika Makazi yake ya Karen katika Kaunti ya Nairobi ambapo alishirikisha zaidi ya wanachama 3,000 wa Wamama wa Hustler, kikundi ambacho kimejitolea kukuza Uchumi wa Bottom-Up

Viongozi waliokuwepo ni pamoja na Gavana wa Kirinyaga Anne Waiguru, wabunge Jayne Kihara (Naivasha Mjini), Millicent Omanga (Aliyependekezwa), Isaac Mwaura (Aliyependekezwa), Patrick Wainaina (Thika) na George Theuri (Embakasi Magharibi).