Nakuru kuwa jiji la nne nchini Kenya

Muhtasari
  • Nakuru imekuwa jiji la nne nchini Kenya!Rais Uhuru aliikabidhi hadhi ya jiji hilo kwa Manispaa ya Nakuru siku ya Jumatano
Image: PSCU

Nakuru imekuwa jiji la nne nchini Kenya!Rais Uhuru aliikabidhi hadhi ya jiji hilo kwa Manispaa ya Nakuru siku ya Jumatano.

Uhuru alitia saini dondoo hilo huku bendera ya Nakuru ikizinduliwa. Nakuru inashika nafasi ya nne baada ya miji ya Nairobi, Kisumu na Mombasa.

Aliandamana na kinara wa chama cha ODM Raila Odinga, spika wa seneti Ken Lusaka miongoni mwa wengine.

Sheria ya Maeneo ya Mijini na Miji inalenga kutekeleza Kifungu cha 184 cha Katiba kinachotoa uainishaji, utawala na usimamizi wa maeneo ya mijini na miji.

Kabla ya kuainishwa kama jiji, maeneo ya mijini lazima yawe na vifaa vya miundombinu kama vile barabara, taa za barabarani, masoko, vituo vya zima moto, utupaji taka na uwezo wa kudhibiti majanga.

Sheria inaonyesha kwamba lazima pia wawe na mipango jumuishi ya maendeleo na kuonyesha uwezo wa kuzalisha mapato ya kutosha ili kuendeleza shughuli.