Kila mwanafunzi wa Shule ya Upili ya Jamhuri kulipa Sh13,385 baada ya bweni kuteketea

Muhtasari
  • Kila mwanafunzi wa Shule ya Upili ya Jamhuri kulipa Sh13,385 baada ya bweni kuteketea
  • Jumla ya hasara iliyosababishwa na tukio la moto pia inakadiriwa kuwa Sh23.6milioni
  • Shule ilitangulia kugawanya jumla ya gharama kwa idadi ya wanafunzi shuleni
Wanafunzi wa shule ya upili ya Jumhuri waruhusiwa kueda nyumbani baada ya mabweni yao kuteketea kwa moyo
Image: Eric KOkonya

Wazazi wa Shule ya Upili ya Jamhuri watalipa pesa nyingi kutokana na uchomaji moto ulioshuhudiwa katika shule hiyo wiki tatu zilizopita.

Gharama ya jumla ya uharibifu kwenye bweni lililobomolewa katika Shule ya Upili ya Jamhuri inakadiriwa kuwa angalau Sh23milioni.

Katika barua iliyoonekana na gazetti la the Star, wazazi wote wanapaswa kuandamana na wanafunzi shuleni.

Wanafunzi wataendelea kwa awamu kuanzia kidato cha nne, kidato cha kwanza, kidato cha tatu na kidato cha pili kwa mfuatano huo.

Bweni lililokuwa na kidato cha pili lilishika moto usiku wa Jumapili mnamo Novemba,15.

Moto huo uliteketeza bweni hilo linalohifadhi wanafunzi wasiopungua 225 na vitanda viliteketea kabisa miongoni mwa vitu vingine.

“Taarifa ya Wizara ya Uchukuzi na Miundombinu, Nyumba, Maendeleo ya Miji na Kazi za Umma kuhusu ukumbi ulioungua uliokuwa na wanafunzi 225 inaeleza kuwa uharibifu ni mkubwa na itahitaji tathimini zaidi ili kupata hati ya malipo.Hata hivyo ripoti ya awali ya QS ni Sh17milioni. ," barua hiyo inasomeka.

Kulingana na shule hiyo, jumla ya vitu vilivyoharibiwa vya wanafunzi vinakadiriwa kuwa Sh4.7milioni.

"Gharama ya double-decker 113 ni Sh1.5milioni, kompyuta zilizoharibika ni Sh250,000, CCTV zilizoharibika na taa za sola ni Sh110,000," inasomeka barua hiyo. .

Gharama ya jumla ya kukarabati bweni hilo inakadiriwa kugharimu ShSh17milioni.

Jumla ya hasara iliyosababishwa na tukio la moto pia inakadiriwa kuwa Sh23.6milioni.

Shule ilitangulia kugawanya jumla ya gharama kwa idadi ya wanafunzi shuleni.

Hii inaashiria kuwa kila mwanafunzi atalazimika kulipa Sh16,985, kiasi kitakacholipwa kupitia wasamaria wema na akiba ya unga ni Sh3,600 kwa kila mwanafunzi.

Katika kuripoti, wanafunzi wote wanatarajiwa kulipa Sh13,385 na kufuta malimbikizo yote ya shule.

Hata hivyo, wanafunzi wote ambao mali zao ziliteketezwa watapewa vitanda na sare za shule za msingi.

Barua hiyo ilitiwa saini na Katibu wa Bodi ya Usimamizi Fred Awuor.

Chanzo cha moto huo hakijajulikana lakini kulikuwa na dhana za wanafunzi 'kuchoka'.

Baadhi ya wazazi pia walidai kuwa wanafunzi walionyesha dalili za machafuko wiki mbili kabla ya moto huo lakini uongozi ukapuuza.

Walidai baadhi ya wanafunzi walirudishwa nyumbani kwa karo ili kupunguza mvutano huo.