logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Drake awapa watu pesa barabarani kama zawadi ya Krismasi

Kupitia ukurasa wake wa Instagram aliweka video mfupi ambayo ilikuwa inaonyesha  Rapa huyo mzawa wa Canada, alitumia siku ya sherehe za Krismasi kugawa pesa  kwa watu wa wakao.

image
na

Habari28 December 2021 - 08:45
Mwanamuziki DRAKE

Mwanamuziki sifika duniani Drake Graham almaarufu Drake, siku ya Jumapili akiwa maeneo ya Toronto nchini Canada alionekana akigawa pesa barabarani nchini humo.

Katika ukurasa wake wa Instagram rapa huyo mzaliwa wa Canada alipakia video fupi ambayo ilionyesha akitumia siku yake ya Krismasi kugawa pesa  kwa wakazi.

Video mbili  ambazo alipakia Instagram akigaawa pesa   siku ya Krismasi zilidhirisha upendo mkubwa anao kwa mashabiki wake.

Mwanamuziki huyo ambaye nyimbo zake zinapendwa dunia nzima kwa mtindo wake wakuimba amevutia wengi kwa kitendo hicho cha hisani 

Hata hivyo haijabainika kiwango cha pesa  msanii huyo wa Kimataifa alitumia siku hiyo ya Boxing Day kutunuku watu waliokuwa Barabarani wakati alipokuwa akipita. 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved