Mwalimu mkuu ajitoa uhai Kitui, alaumu mkewe kwa kumsukuma hadi kifo

Muhtasari

•Kupitia kwa barua yake marehemu alimshtumu mkewe ambaye amekuwa akizozana naye kwa kuwachochea watu wote walio karibu naye kumchukia, wakiwemo watoto wao.

Gari la polisi lililobeba mwili wa marehemu mwalimu. Maafisa wa upelelezi walikuwa wametembelea nyumbani kwa marehemu katika kijiji cha Itumbi.
Gari la polisi lililobeba mwili wa marehemu mwalimu. Maafisa wa upelelezi walikuwa wametembelea nyumbani kwa marehemu katika kijiji cha Itumbi.
Image: DENSON MUTUTO

Mwalimu mkuu wa shule moja ya msingikatika eneo la Mwingi, kaunti ya Kitui alijitoa uhai na kuacha kama ameandika barua akimlaumu mkewe kwa kumsukuma hadi kutamatisha maisha yake.

Akithibitisha kisa hicho, OCPD wa Mwingi, Peter Mutuma alisema kuwa mwalimu mkuu wa shule ya msingi ya Wikithuki Jacob Nguli alijitoa uhai katika kijiji cha Ithumbi, kaunti ndogo ya Mwingi ya kati, Kitui.

Kupitia kwa barua yake marehemu alimshtumu mkewe ambaye amekuwa akizozana naye kwa kuwachochea watu wote walio karibu naye kumchukia, wakiwemo watoto wao.

“Siku zote umekuwa ukiniwazia vibaya, hujawahi kunithamini bila kujali jitihada nilizofanya ili kuhudumia familia,”sehemu ya barua iliyoachwa na marehemu ilisoma.

Kakake, David Nguli, alidai kuwa kila wakati marehemu alipokuwa na dhiki, alikuwa anamfungukia akiongeza kuwa mke wake ndiye wa kulaumiwa kwani alimpa msongo wa mawazo sana.

Aidha alifichua kuwa mke wa marehemu alienda nyumbani kwa wazazi wake ambako ndiko anakoishi kufuatia ugomvi wa kinyumbani uliotokea na kumwacha Nguli peke yake.

Katibu mtendaji wa Chama cha Kitaifa cha Walimu Kenya (KNUT), tawi la Mwingi, Mike Mbutu alitembelea familia ya marehemu ili kuwasilisha rambirambi zake na kusema kuwa chama hicho kitashirikiana na TSC kuhakikisha walimu wanapewa usaidizi wa kisaikolojia.

Aidha alisema marehemu alikuwa mwalimu na aliwahi kuwa mwalimu mkuu kwa zaidi ya miaka kumi.

Mbutu aliitaka Serikali kulishughulikia suala la ugatuzi kwa kuzingatia umri wa mwalimu akidai kuwa sera hiyo haina manufaa kwa walimu.

(Utafsiri: Samuel Maina)