Mtangazaji wa zamani wa runinga ya Citizen Hussein Mohammed ateuliwa kuwa mkuu wa mawasiliano wa DP William Ruto

Muhtasari
  • Aliyekuwa mtangazaji wa runinga ya Citizen Hussein Mohammed ateuliwa kuwa mkuu wa mawasiliano wa DP William Ruto
DP Ruto na Hussein Mohammed
Image: DPPS

Aliyekuwa mtangazaji wa runinga ya Citizen Hussein Mohamed ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mawasiliano wa Naibu Rais William Ruto.

Atakuwa msimamizi wa mawasiliano ya kampeni za urais za Ruto kabla ya uchaguzi wa Agosti 9.

DP Ruto alimkaribisha rasmi Hussein katika kambi yake baada ya kukutana naye katika makazi yake rasmi ya Karen.

"Hussein Mohamed, mwanahabari maarufu wa TV, ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mawasiliano katika Kampeni ya Urais ya William Ruto. Karibu kwa timu ya Hustler," DP alisema.

Baada ya kuondoka kwenye runinga ya Citizen, Hussein amekuwa akifanya kazi kama mshauri wa mawasiliano na NGOs.

Mwanahabari maarufu wanasifika kwa ufasaha wake na mahojiano magumu ya televisheni.

Kujiondoa kwake kwenye vyombo vya habari kulizua taharuki miongoni mwa Wakenya waliofurahia mtindo wake wa kuwahoji wageni wa kisiasa nchini.