Kalonzo akanusha madai ya kujiunga na UDA

Muhtasari

• Kinara wa Wiper Kalonzo Musyoka amefutilia madai kwamba kuna uwezekano wake kujiunga na naibu rais William Ruto mbele ya uchaguzi wa Agosti 9.

• “ Nishafanya uamuzi tayari, hakuna mkenya ambaye anapaswa kufikiria kwamba mimi Kalonzo nitafanya kazi na William Ruto,” Kalonzo alisema.

Twitter KWA HISANI
Twitter KWA HISANI
Image: Kalonzo Musyoka

Kinara wa Wiper Kalonzo Musyoka amefutilia madai kwamba kuna uwezekano wake kujiunga na naibu rais William Ruto mbele ya uchaguzi wa Agosti 9.

Matamshi hayo yalijiri siku moja tu baada ya taarifa aliyoitoa kuhusu kuwepo kwa uwezakano wake kushirikiana na Raila Odinga tena licha ya Odinga kutoheshimu makubaliano yao ya 2017 chini ya muungano wa NASA.

“ Nishafanya uamuzi tayari, hakuna mkenya ambaye anapaswa kufikiria kwamba mimi Kalonzo nitafanya kazi na William Ruto,” Kalonzo alisema.

Musyoka aliongeza kwamba uamuzi huo wa kutoungana na Ruto umetokana na mashauriano aliyoyafanya na wanachama wa Wiper na viongozi wa Muungano wa OKA.

Vilevile alisisitiza kwamba OKA haijafanya mazungumzo yoyote na katu muungano huo hautajiunga na kambi ya UDA.

“Hatuliwazii kabisa. OKA haiwezi kujiunga na UDA,” Kalonzo alisisitiza.

Aidha Kalonzo alisema kwamba OKA bado iko imara licha ya taarifa yake ya kutaka kushirikiana na kiongozi wa ODM, Raila Odinga kwa mara nyingine tena.

“Bado tuko imara.Rafiki yangu wa KANU Gideon Moi sasa ni kama pacha wangu,” alisema.

Musyoka aliweka wazi kwa,mba viongozi walio chini ya muungano wa OKA walitarajiwa kutia sahihi vyeti ambavyovitaurasmisha muunga huo, mbele ya mazungumzo na muungano wa Azimio.

 

Click here to edit this text.