Uhuru awapongeza Eliud Kipchoge na Brigid Kosgei baada ya ushindi katika mbio za Tokyo

Muhtasari
  • Uhuru awapongeza Eliud Kipchoge na Brigid Kosgei baada ya ushindi katika mbio za Tokyo
  • Tamirat Tola wa Ethiopia alikuwa wa tatu kwa 2:04:14.

Eliud Kipchoge baada ya kushinda dhahabu usiku wa kuamkia Jumapili
Eliud Kipchoge baada ya kushinda dhahabu usiku wa kuamkia Jumapili
Image: HISANI

Rais Uhuru Kenyatta amewapongeza mshikilizi wa rekodi ya dunia ya mbio za marathon Eliud Kipchoge na Brigid Kosgei baada ya ushindi wao katika mbio za Tokyo.

"Uhuru amewapongeza Kipchoge na Kosgei kwa uchezaji wao bora katika mbio zao za Tokyo Marathon 2021," Ikulu ilisema Jumapili.

Uhuru alisema wawili hao walitawala mbio zao huku wakiweka nyakati za kasi zaidi kuwahi kukimbia katika ardhi ya Japan katika mbio zao mtawalia.

Kipchoge Bingwa wa Olimpiki mara mbili alishinda mbio hizo kwa muda wa saa 2: 02: 40 huku Brigid ambaye anashikilia rekodi ya Dunia akikamilisha mbio kwa saa 2:16.02.

Kipchoge alikimbia marathoni ya tatu kwa kasi zaidi maishani mwake—na ya nne kwa kasi zaidi katika muda wote.

Kipchoge anashikilia rekodi ya dunia, 2:01:39, aliyoweka 2018 mjini Berlin, na pia alikimbia 2:02:37 mwaka wa 2019 jijini London.

Amos Kipruto ambaye alimsukuma Kipchoge kwa takriban maili 22, alikimbia kibinafsi kwa sekunde 17 na kumaliza wa pili kwa 2:03:13.

Tamirat Tola wa Ethiopia alikuwa wa tatu kwa 2:04:14.

Hapo awali, Kipchoge aliomba ulimwengu kuungana huku akitoa ushindi wake wa marathon wa Tokyo kwa amani.

Kipchoge alishinda mbio za Tokyo Marathon katika rekodi mpya ya mwendo wa saa 2:02:40 Jumapili asubuhi nchini Japan.