Naibu rais William Ruto amewapokea wajumbe wa bunge la kaunti zaidi ya 40 kutoka kaunti za Meru na Tharaka Nithi.
Wajumbe hao wote wanasemekana kukiasi chama tawala cha Jubilee na kujiunga na kile cha naibu rais cha UDA kama njia moja ya kujihakikishia nafasi nzuri kuelekea uchaguzi mkuu wa Agosti 9.
Hatua hii inakuja siku mbili tu baada na naibu rais kuwapokea katika chama cha UDA tena wajumbe wa kaunti ya Kiambu zaidi ya 30 waliochaguliwa kwa kupigiwa kura kupitia chama tawala cha Jubilee ambacho kinaendelea kutorokwa na wengi huku wakionekana kuwa na upendeleo mkubwa kwa chama kipya kabisa cha UDA.
Ruto anatarajiwa kutangazwa rasmi kesho kama mgombea urais wa chama hicho baada ya kamati ya uchaguzi ya chama ch UDA kumpitisha bila kupingwa wikendi iliyopita.
Atamenyana na mwenzake kutoka muungano wa Azimio la Umoja Raila Odinga katika uchaguzi wa Agosti 9.