Kenya yataka wanajeshi wa Afrika Mashariki kutumwa DR Congo

Muhtasari

•Rais Kenyatta ametoa wito wa kutumwa kwa kikosi cha kanda ya Afrika Mashariki ili kurejesha usalama katika maeneo yenye matatizo ya mashariki mwa DRC.

•Tangu mwezi Machi, mapigano kati ya jeshi la Congo na waasi wa M23 yamewakosesha makazi zaidi ya watu 80,000.

Mapigano katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo yamesababisha maelfu ya raia kukimbia makazi yao
Mapigano katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo yamesababisha maelfu ya raia kukimbia makazi yao
Image: BBC

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ametoa wito wa kutumwa kwa kikosi cha kanda ya Afrika Mashariki ili kurejesha usalama katika maeneo yenye matatizo ya mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Katika taarifa yake, pia alitoa wito wa “kusitishwa mara moja kwa uhasama wote kwa makundi yote yenye silaha, ya kigeni na ya ndani, kuweka silaha chini mara moja na bila masharti’’ huku kukiwa na mapigano makali katika wiki za hivi karibuni.

Jeshi la Kanda ya Afrika Mashariki litatumwa mara moja katika mikoa ya Ituri, Kivu Kaskazini na Kusini ili kutekeleza amani kwa kushirikiana na vikosi vya Umoja wa Mataifa (Monusco), alisema uamuzi wa kuanzisha kikosi cha kikanda ulifanyika Aprili wakati Bw Kenyatta, mwenyekiti wa sasa wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, aliwakaribisha marais wa kanda kuhusu mgogoro wa DR Congo ambao pia unatishia nchi jirani.

Zaidi ya vikundi 100 vya ndani na nje vinafanya kazi katika majimbo ya Kivu Kusini, Kivu Kaskazini na Ituri na vimevuruga eneo hilo kwa zaidi ya miongo miwili.

Tangu mwezi Machi, mapigano kati ya jeshi la Congo na waasi wa M23 yamewakosesha makazi zaidi ya watu 80,000.

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imeishutumu Rwanda kwa kuunga mkono kundi linaloundwa na Watutsi wa asili ya Congo, lakini serikali ya Kigali inakanusha tuhuma hizo