Umati Wamfuata Didmus Barasa baada ya Kunyimwa Fursa ya Kuzungumza

Muhtasari

•Barasa alikuwa ameitwa kuhutubia umati, lakini hotuba yake ilikatizwa, na mabishano yakazuka kati yake na mkuu wa hafla.

 

Kimilili MP Didmus Barasa
Kimilili MP Didmus Barasa
Image: HISANI

Mbunge wa Kimilili Didmus Barasa kwa mara nyingine amejipata pabaya baada ya kunyimwa nafasi ya kuzungumza katika hafla iliyofanyika eneo bunge lake la Kimilili, kaunti ya Bungoma.

Mnamo Jumamosi, Juni 25, Barasa alilazimika kujiondoa katika hafla ya kisiasa iliyoandaliwa na wapinzani wake katika kaunti ya Bungoma baada ya kunyimwa nafasi ya kuzungumza.

Barasa alikuwa ameitwa kuhutubia umati, lakini hotuba yake ilikatizwa, na ugomvi ukazuka kati yake na mfawidhii, ambaye alionekana kutofurahishwa na kile Barasa alitaka kusema.

Baadaye mfawidhii alichukua kipaza sauti chake, na mbunge akatoka nje kwa hiari akiwaaga umati uliokusanyika.

Lakini wafuasi wake waliondoka na  mbunge  huo kama ishara ya kuonyesha mapenzi yao kwake walimfuata huku wakilitaja jina lake.

Hafla hiyo ambayo ilidaiwa kuandaliwa na washirika wa Gavana wa Bungoma Wycliffe Wangamati ilikamilika ghafla baada ya mbunge huyo kuondoka, akifuatwa na mamia ya wafuasi wake.

Barasa alisema umati uliomfuata ulichochewa na hisia za mshikamano, upendo na heshima kwake.

Baadaye, akiwahutubia wakazi, alikashifu kisa hicho huku akipigia debe uungwaji mkono kwa azma yake na ya mgombeaji wa Kenya Kwanza Kenneth Lusaka.

Spika Ken Lusaka atachuana na mwaniaji Wycliffe Wangamati.

"Uliona watu hao wakijaribu kunisukuma, lakini mara tu nilipotoka kwao, ulinifuata. Kwa hivyo nyote mnafanya kazi nzuri, na ninawapongeza kwa hilo," Barasa alisema

Aliwahakikishia wakazi enzi mpya pindi Lusaka atakapochaguliwa kuwa gavana wa kaunti ya Bungoma.