Mfumo maalum wazinduliwa kuwadhibiti wanaokiuka sheria za barabarani

Majaribio yamefanyika Kwenye barabara ya magharibi ya Outering

Muhtasari

•Sekta ya uchukuzi imezindua  mbinu mpya ya kuwanasa wale wasiozingatia sheria zilizowekwa barabarani.

•Mhandisi huyo alisema kuwa kuna majaribio ambayo yamefanyika hapa nchini kwenye barabara ya magharibi ya Outering 


Thika-Road-Jam
Thika-Road-Jam
Image: MAKTABA

Sekta ya uchukuzi imezindua  mbinu mpya ya kuwanasa wale wasiozingatia sheria zilizowekwa barabarani.

Washikadau katika mkutano uliofanyika KICC, walipongeza Polisi wa trafiki kwa kazi nzuri ya kuhakikisha kuwa Wakenya wapo salama wanapotumia  barabara kwa kuhakikisha wanazingatia sheria za trafiki.

''Ningependa kuongeza kwamba kando na Polisi na wamiliki wa magari kuhakikisha wanatumia barabara vizuri, tunahitaji pia kuhusisha teknolojia ya kisasa kwa madhumuni ya utekelezaji wa sheria za trafiki,'' Oginga alisema.

Mhandisi huyo alisema kuwa kuna majaribio ambayo yamefanyika hapa nchini kwenye barabara ya magharibi ya Outering  ambapo teknolojia hizo  almaarufu E Police zimeanza kutumika.

''E Police inauwezo wakunasa gari  kwenye kamera ukiwa unatumia barabara  vibaya na kusambaza taarifa hizo kwa kituo cha usimamizi wa trafiki na kwa hilo utashtakiwa kwa kosa hilo'' aliongeza.

Alisema kuwa  wanatazamia kuweka  mfumo huo katika barabara zote ili kusaidia katika kudhibiti sheria za usafiri ambao umekuwa tatizo kubwa  nchini.

''Pia kutawekwa vidhibiti mwendokasi barabarani ili kuepusha suala la maafisa kutoka NTSA kujificha kwenye kichaka kupima ukomo wa mwendo kasi wa magari mbalimbali'' Oginga alisema.

Teknolojia hiyo mpya itaweza kutambua usajili wa magari na kumuonya dereva juu ya mwendokasi ili utakapokamatwa  na Polisi  hatakuwa na malalamishui kwa kuwa alishapewa tahadhari mapema na mfumo hiyo mpya.