Rasmi! Nyama choma, Chapo, Chips Mayai zaingia kwenye kamusi

Maneno 'Sambaza' na 'kuweka lami' pia yametambulika kwenye kamusi

Muhtasari

•Nyama Choma ni mojawapo ya maneno 200 mapya yaliyoongezwa katika toleo lililoboreshwa la  Kamusi ya Kiingereza ya Oxford (OED).

•Maneno mengine yaliyoongezwa ni kama, sambaza maana yake "kushirikisha au kutuma kitu"  na kuweka lami kumaanisha "kitendo au mchakato wa kutembea mitaani kutafuta kazi".

Nyama Chom kwa viazi
Image: BBC

Kutembelea Kenya bila kuonja ladha ya nyama choma basi safari yako haijakamilika, sasa unaweza kuitafuna nyama huku ukijua kwamba waandishi wa kamusi kutoka Oxford wameiweka katika kamusi yao ya Kiingereza ambayo maarufu duniani.

Ni mojawapo ya maneno 200 mapya yaliyoongezwa kutoka katika lugha ya Afrika Mashariki katika toleo lao lililoboreshwa la hivi karibuni la Kamusi ya Kiingereza ya Oxford (OED).

Kamusi ya Oxford ni moja ya vyanzo vinavyoheshimiwa sana vya lugha.

Maneno mengine ambayo sasa yanatambulika katika kamusi ni:

chapo - chapati nyembamba

chips mayai – kwa Tanzania na Kenya –viazi vya kukaanga vilivyochanganywa na mayai wakati wa kupika.

katogo - jina la mlo wa kawaida ambao ni kifungua kinywa cha asubuhi nchini Uganda unaojumuisha matoke iliyochemshwa kwenye sufuria na viungo vingine mbalimbali.

Mbali na hayo maeneo mengine ni kama, sambaza maana yake "kushirikisha au kutuma kitu" sasa iko kwenye kamusi hiyo ya Oxford pamoja na kuweka lami (tarmacking) ambayo ni "kitendo au mchakato wa kutembea mitaani kutafuta kazi".

Kama unashirikiana kufanya kazi na mtu unaweza kuiita collabo kwa kujua kwamba ni Kiingereza sahihi. Na ikiwa ungependa kusherehekea kuingizwa kwa maneno haya basi unaweza kupiga kelele "oyee!" – neno ambalo kwa mujibu wa wataalam wa kamusi ni njia ya kueleza "kutia moyo au kuunga mkono”