Maafisa 5 wa polisi wamejeruhiwa baada ya kuvamiwa na watu wenye silaha

Haya yanajiri miezi sita baada ya mlipuko wa matatu kuua watu saba katika kaunti hiyo.

Muhtasari

•Maafisa watano wa polisi walijeruhiwa baada ya watu wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wa Al Shabaab kuwavamia maafisa  hao wa usalama siku ya Ijumaa.

Mafisa wa polisi wakishika doria katika eneo la Lamu
Mafisa wa polisi wakishika doria katika eneo la Lamu
Image: MAKTABA

Maafisa watano wa polisi walijeruhiwa baada ya watu wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wa Al Shabaab kuwavamia maafisa  hao wa usalama siku ya Ijumaa.

Maafisa hao wa usalama walikuwa wakishika doria huko Mandera kusini wakati kisa hicho kilipotokea.

Haya yanajiri miezi sita baada ya mlipuko wa matatu kuua watu saba katika kaunti hiyo.

Kulingana na ripoti ya polisi, watu hao wenye silaha pia walirusha guruneti lililorushwa kwa roketi mara baada ya mlipuko huo.

 

Uvamizi huu unasawiana na taarifa kuhusu usalama huko Molo wiki moja uliopita  ambapo  ilihofia kuwa kuna uwezekano wa makundi haramu eneo hiyo.

Katika  operesheni iliyofanyika ya kuwafurusha katika maeneo hiyo huenda uliwafanya wahalifu hao kuhamia mashinani.

Kulingana na Kamishna Msaidizi wa Kaunti Ndogo ya Molo Steve Ondote kuongezeka kwa ukosefu wa usalama katika vijiji vya Mooto na Mutirithia ni jambo la kutisha na kuwahakikishia wakazi wa eneo hilo usalama wao kwani wamejitolea kurejesha usalama katika eneo hilo.