logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mshukiwa wa ujambazi auawa huku polisi wakiimarisha doria kukabili utovu wa usalama

Mshukiwa alipigwa risasi alipokuwa akijaribu kutoroka maafisa wa polisi akiwa na wenzake.

image
na Davis Ojiambo

Habari16 November 2022 - 13:37

Muhtasari


  • • Polisi walipata panga mbili, bunduki ya kujitengenezea nyumbani na simu ambazo zinaaminika kuibwa kwa wananchi.

Mshukiwa wa ujambazi aliyekuwa amejihami aliuawa kwa kupigwa risasi mjini Thika na polisi usikuwa kuamkia leo huku idara ya polisi ikiimarisha doria kudhibiti hali ya usalama nchini.  

Kulingana na maelezo ya idara ya DCI jambazi huyo alikuwa miongoni mwa genge la washukiwa watatu ambao wamekuwa washambulia watu kwenye barabara ya Cascade Premier.

Mshukiwa alipigwa risasi alipokuwa akijaribu kutoroka maafisa wa polisi.

 "Tukio hilo liliwafanya majambazi wengine ambao walikuwa wamejihami kwa panga na bunduki kutoroka . Polisi walifanikiwa kumtia mbaroni mshukiwa mmoja huku mwenzake akitoroka ," DCI walisema.

Polisi walipata panga mbili, bunduki ya kujitengenezea nyumbani na simu ambazo zinaaminika kuibwa kwa wananchi.

Pikipiki isiyo na nambari ya usajili iliyokuwa ikitumiwa na majambazi hao pia ilinaswa na maafisa.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved