logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Ruto: Katika siku 12, tayari Ksh 1.2Bn za Huster Fund zimerudishwa na wakopaji

Katika siku 12, Hustler Fund imekopesha Ksh bilioni 7.5 kwa watumiaji milioni 15.4 - Ruto.

image
na Davis Ojiambo

Habari12 December 2022 - 10:17

Muhtasari


  • • Zaidi ya Ksh milioni 400 zimeokolewa na Wakenya kutoka kwa Hazina hiyo - rais alisema.
Ruto aipigia debe Huster Fund

Rais William Ruto sasa ametoa takwimu za kustaajabisha jinsi Wakenya wengi wamekuwa wakichukua mkopo wa Hustler Fund katika siku 12 tu tangu mkopo huo kuzinduliwa mnamo Desemba 1.

Rais alisema kuwa wakenya zaidi ya milioni 14 tayari waliotuma maombi ya kutaka mkopo huo wameshapewa na tayari mikopo ipatayo zaidi ya bilioni 7 imetolewa na serikali kwa wapambanaji wa chini ambao alisema wanatarajiwa kuanzisha biashara ndogo ndogo za kujikimu katika uchumi huu ambao umefumuka pakubwa.

"Katika siku 12, Hustler Fund imekopesha Ksh bilioni 7.5 kwa watumiaji milioni 15.4 kwenye jukwaa hilo," Rais William Ruto amesema.

Aidha, rais Ruto pia alisema kuwa tayari riba ya zaidi ya milioni 400 imepatikana kutokana na wale ambao wamekuwa wakirudisha mikopo hiyo, hivyo kuwatupia dongo machoni wale ambao wamekuwa wakisema kuwa mkopo wa Hustler Fund hautafaulu kwani watu wanachukua na hawawezi kurudisha – kumbe kweli watu wanarudisha eeh!

“Zaidi ya Ksh milioni 400 zimeokolewa na Wakenya kutoka kwa Hazina hiyo, zaidi ya Ksh bilioni 1.2 zimerejeshwa na wakopaji,” alisema rais.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved