Shirika la fedha duniani (IMF) limeidhinisha mkopo wa shilingi bilioni 55.1 (sawa na dola milioni $447.39) kwa Kenya.
Mkopo huo ni sehemu ya nne ya mkopo wa bilioni shilingi bilioni 288 ($2.34 bilioni) unaotolewa kwa kipindi cha miezi 38 ambao uliidhinishwa mwezi Aprili mwaka jana.
Mkopo huo mpya unapelekea pesa zilizotolewa chini ya mpango wa miaka mitatu kufikia jumla ya shilingi bilioni 203.8 (dola bilioni $1.656 ) baada ya mpango wa tathmini ya nne ya ufadhili huo wa muda mrefu (EFF) na mkopo wa muda mrefu (ECF) baina ya IMF na Kenya Kenya.
IMF inatarajia ukuaji wa uchumi wa Kenya kwa asilimia 5.3 mwaka huu na mfumuko wa bei wa 7.7 katika kipindi cha mwaka huu wa 2022.