Mkenya akamatwa kuhusika na shambulio lilioua 17 DR Congo

Takribani watu 17 walifariki na wengine zaidi ya 30 kujeruhiwa katika s

Muhtasari

•Msemaji wa jeshi la kanda ya DR Congo Kapteni Anthony Mualushayi alisema mshukiwa alikamatwa katika kituo cha mpakani cha Kasindi muda mfupi baada ya shambulio hilo.

Image: BBC

Raia wa Kenya amekamatwa kwa kuhusishwa na shambulio la mlipuko wa bomu kwenye kanisa moja huko Kasindi katika Jimbo la Nord Kivu Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Msemaji wa jeshi la kanda ya DR Congo Kapteni Anthony Mualushayi alisema mshukiwa alikamatwa katika kituo cha mpakani cha Kasindi muda mfupi baada ya shambulio hilo.

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Felix Tshisekedi amelaani vikali shambulio hilo na kuahidi kuwafikisha wahalifu mbele ya sheria.

Takribani watu 17 wamefariki dunia na wengine zaidi ya 30 kujeruhiwa kutokana na mlipuko wa bomu hapo jana mchana wakati wa ibada huko Lubiriha katika wilaya ya Beni mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Waasi wa ADF wanaendelea kuwa tishio kwa usalama wa raia wanaoishi mashariki mwa DRC. Shambulio hilo ambalo tangu wakati huo limedaiwa na waasi wa kiislamu-IS inayojiita Jimbo la Afrika ya Kati (ISCAP).