logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mtoto aliyefariki na kuzikwa wiki chache ziilizopita aonekana akiwa hai katika kijiji tofauti.

Polisi walifukua kaburi lake na wazazi wakasema hawamtamui maiti bali wanamtambua mwanao aliye hai.

image
na Davis Ojiambo

Habari01 May 2023 - 05:05

Muhtasari


  • • Polisi walifukuwa mwili huo na kuondoka nao kwa uchunguzi zaidi kubainini wa nani.
Mwili wa mtoto huyo aliyedhaniwa kuwa yeye ulifukuliwa.

Kulikuwa na hali ya sintofahamu katika Kijiji kimoja kaskazini mwa taifa jirani la Tanzania, mkoani Mwanza baada ya mtoto anayedaiwa kufariki na kuzikwa kuonekana akitembea katika kijiji jirani.

Kulingana na taarifa hiyo ya kustaajabisha iliyopeperushwa na runinga ya East Africa, mtoto huyo aliyetambuliwa kwa jina Mabilika Wilson anasemekana kuzikwa Aprili 17 lakini mnamo Aprili 27,2023 majira ya saa ya saa 12(18:00) jioni katika Kijiji cha Mwangika, Kata ya Mwabomba, Tarafa ya Ngulla ,Wilaya ya Kwimba, mtoto huyo alionekana tena akitembea katika kijji hicho jirani.

Mtoto huyo alikuwa na miaka 8 mpaka kifo chake.

Taarifa hizo zilifanyiwa kazi kwa haraka ambapo Askari Polisi waliweza kumpata baba Mzazi wa mtoto huyo aitwaye Wilson Bulabo(35) pamoja na mama wa mtoto aitwaye Helena Robert(33) wote Wakulima na Wakazi wa Salong’we -Magu.

Wazazi hao waliweza kumtambua kuwa ni mtoto wao ambaye alifariki Aprili 16,2023 muda wa saa 6:00(12:00) mchana kwa maradhi na kuzikwa Aprili 17,2023 majira ya saa 8:00(14:00) mchana huko Kijiji cha Salong’we, Kata ya Mwamabanza ,Tarafa na Wilaya ya Magu.

Baada ya mkanganyiko huo, Jeshi la Polisi kwa kuhusisha wataalam mbalimbali lililazimika kufukua kaburi ambalo alizikwa Mabilika Wilson ili kuweza kujiridhisha kama kulikuwa na mabaki ya mwili wa mtoto huyo.

Ambapo baada ya kufukua mwili huo wazazi walisema kuwa ule mwili sio wa mtoto wao bali wanamtambua yule aliyeokotwa Wilaya ya Kwimba kuwa ndiye wao.

Hivyo, mwili huo umechukuliwa kwa ajili ya uchunguzi kujua chanzo cha kifo chake pia kuchunguza yule mtoto aliyeokotwa kisha kutambuliwa na wazazi wao kuwa ni mtoto wao na kutambua jambo lililojifucha nyuma ya kifo cha mtoto huyo.

Tukio sawa na hilo liliripotiwa katika kijiji cha Nyaboterere kaunti ya Kisii ambapo mwanabodaboda aliyefungwa jela kwa mwezi mmoja alirejea nyumbani na kupata familia yake ilikuwa imezika mwili tofauti wakidhani ni yeye.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved