logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Ruto alalamika Wakenya kukataa kulipa Hustler Fund, "Wengine wamehama na pesa!"

Rais alitoa onyo kali akisema, 'tutakutana huko mbele' kwa walle wasiolipa.

image
na Davis Ojiambo

Habari27 May 2023 - 11:19

Muhtasari


  • • Rais alisema kuwa awamu ya pili itazinduliwa Juni mosi na kiwango chake kitakuwa kuanzia elfu 20 hadi 200.
Ruto atoa onyo kali kwa wale wanaochukua Hustler Fund na kuhama.

Rais William Ruto amelalamika vikali idadi kubwa ya Wakenya waliochukua mkopo wa Hustler Fund na kukataa kulipa.

Akizungumza katika kaunti ya Embu Ijumaa, mkuu wa taifa alisema kuwa kuna watu wengine ambao walikuwa katika mkutano huo na ambao wamekataa kulipa na sasa hawakuwa wanataka kumwangalia moja kwa moja usoni.

Rais alisema kuwa awamu ya pili ya mikopo ya Hasoal itarudi hivi karibuni lakini akasisitiza kwamba wengi hawajalipa awamu ya kwanza na kudai kuwa kuna baadhi yao wamehama nchini wakiwa na mkopo huo.

Alitoa onyo kali kwa wale ambao wamekataa kulipa akisema kuwa ‘tutakutana hapo mbele’.

“Kuna watu wengine hapa wamehama na pesa za Hastler Fund. Mimi nikiona watu wengine hapa hawataki kuniangalia kwa macho vizuri kwa sababu wako na deni langu, nyinyi. Tutakutana hapo mbele. Unajua kuna jamaa alisema eti wacha tuchukue hii ya Ruto kwa sababu tulimpigia kura, hapana,” rais alisema.

Rais Ruto alisema kuwa awamu ya pili ya mikopo ya Hasola itazinduliwa Alhamisi Juni mosi wakati wa sherehe za Madaraka ambazo zitafanyika katika kaunti hiyo ya Embu.

Pia mkuu wa taifa aliahidi kwamba safari hii kiwango kitaongezeka kidogo na hakitakuwa shilingi mia tano kama ilivyokuwa katika awamu ya kwanza.

“Awamu ya pili ya Hasola Fund itazinduliwa hapa Alhamisi, kwa wale wafanyibiashara mjipange. Haitakuwa shilingi ile mia tano, elfu moja, elfu mbili. Sasa tunakuja kuanzisha awamu ya pili ambapo utapata kuanzia elfu 20 hadi elfu 200. Lakini sio pesa mnachukua na kuhama, ni pesa unachukua na kulipa, alaar,” Ruto alisema.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved