Baada ya mmoja wao kutoa hotuba fupi, vijana hao wa Manchester United walibeba jeneza lake mabegani kuelekea katika nyumba yake ya milele alikopumzishwa.
Shosh wa Kinangop alifariki wiki jana baada ya kile kilitajwa kuwa ni kuugua kwa muda.
Ajuza huyo mpaka kifo chake, alikuwa amejizolea umaarufu kwenye mtandao wa video fupi wa TikTok akiwa na wafuasi Zaidi ya laki 6.
Tiktoker mkongwe Zaidi kuwahi kushuhudiwa nchini Kenya, maarufu kwa jina Shosh wa Kinangop alizikwa Jumatatu nyumbani kwake katika kaunti hiyo.
Mcheshi huyo mkongwe ambaye alijizolea umaarufu kutokana na skit zake za kuchekesha akiwa amevalia jezi ya Manchester United alipewa heshima zake za mwisho huku idadi kubwa ya waombolezaji wakiwa wamevalia jezi za timu hiyo ya Uingereza kama njia moja ya kuonesha Shosh wa Kinangop heshima zake za mwisho.
Katika video ambazo zimekuwa zikisambazwa mitandaoni kutoka kwa hafla hiyo ya maziko, mashabiki wanaodhaniwa kuwa wa Manchester United walifurika wakiwa kwenye jezi hizo za rangi nyekundu huku pia wakiwa na bango kubwa lenye nembo ya Manchester United na chini yake ujumbe kwa Shosh Wa Kinangop wakimuomboleza kwamba wataukosa sana ucheshi wake.
Kwa upendo na heshima kubwa, walibeba jeneza lake hadi kando ya kaburi, na kuhakikisha anapumzishwa kwa uangalifu na heshima ya hali ya juu.
Uwepo wao ulionyesha athari kubwa aliyonayo Shosh kwenye jumuiya yake ya mtandaoni, na kuwaunganisha watu wa asili tofauti ili kuheshimu kumbukumbu yake.